LYRICS: NAONA BADO By Sudiboy Ft Amileena

27/06/2014
SUDIBOY ft AMELINA - NAONA BADO 

VERSE 1
Naona bora afadhali nioe mke, basi muwe wawili,
Imepungua yangu imani, wananicheka ona majirani,
Penzi nililokumwagia, utamu wa ndoa unaniishia, (Aaaaaahhh)
Wazazi wanaulizia, mpaka lini watasubiria … Eeeh
Nayaheshimu yako maamuzi, mara mbili fikiria,
Ujana moshi hauna ujuuzi, sote njia tunapitia,
Nayaheshimu yako maamuz, Oooh
Ujana moshi hauna ujuuzi, Mke wangu Eeeh

CHORUS
Naona bado Naona bado, hujaridhia kuishi na mimi
Naona bado Naona bado, ndio maana hutaki kuzaa na mimi
Naona bado Naona bado, hujaridhia kuishi na mimi
Naona bado Naona bado, ndio maana hutaki kuzaa na mimi

VERSE 2: AMELINA
Unaogofya hadharani na matisho za mke wa pili,
Najawa mie na majonzi kwa kujua tena hauniamini,
Naomba uwe na subira, sio eti sitaki kukuzalia, (Aaaaaahhh)
Wakati wetu utafika, tuwe na sisi familia,
Yaheshimu yangu maamuzi, naomba mpenzi wewe subiria
Hili jambo nzito la uzazi, bado mi nalifikiria
Heshimu yangu maamuzi, Oooh
Hili jambo sila ujuzi, bado mi nafikiria

CHORUS 2:
Naomba bado Naomba bado, muda hujafika kuzaa nawe
Naomba bado Naomba bado, subiri kidogo bwana we
Naomba bado Naomba bado, muda hujafika kuzaa nawe
Naomba bado Naomba bado, subiri kidogo bwana we

VERSE 3:
SUDIBOY
Nimejaribu kukwambia, japo tuzae hata mtoto mmoja,
Majibu nimesubiria, sikuelewi daily unasema ngoja,
Unaogopa kupoteza ujana, unataka tuishi kama jana,
Mmh… Eti bado mapema, kifungu gani cha ndoa kimesema,
AMELINA:
Yaheshimu yangu maamuzi, naomba mpenzi wewe subiria,
Hili jambo nzito la uzazi, bado mi nalifikiria,
SUDIBOY:
Nayaheshimu yako maamuz, Oooh
Ujana moshi hauna ujuuzi, Mke wangu Eeeh

CHORUS
SUDIBOY
Naona bado Naona bado, hujaridhia kuishi na mimi
Naona bado Naona bado, ndio maana hutaki kuzaa na mimi
AMELINA:
Naomba bado Naomba bado, muda hujafika kuzaa nawe
Naomba bado Naomba bado, subiri kidogo bwana we

Sudi weeee ….wacha papara
Mda wetu utafikaaa

Watch the Song here:
 
Share on Google Plus

About Anonymous

He is the CEO of Cityville Mombasa. Reach him on 0728622801 or gangsta6g@gmail.com