LYRICS: Maria By Ally B

28/10/2015
Artist: Ally B
Song: Maria
Year: 2010
Language: Kiswahili

Verse 1

Sikilize kwa makini mpenzii
na uyaweke akilini Maria
maisha yetu ni magumu mpenzi
hupasa ufahamu Maria
najua una huzuni mpenzi
sababu ya umaskini lazizi
mi najua una huzuni mpenzi
sababu ya umaskini lazizi

lakini si kosa lako wala si langu
ajuaye kamili hilo ni baba Mungu Maria
lakini si kosa lako wala si langu
ajuaye kamili hilo ni baba Mungu Maria

Chorus
Maria...
Maria vumilia
Maria...
Maria sikia

Verse 2
maisha yetu ya umaskini
iko siku mpenzi tutawini
leo mpenzi tunalala chini
huenda kesho tupo kitandani
jikaze leo twende kwa miguu
kesho tuna gari barabarani
inabidi ukaze moyo Maria
usije niache pweke Maria
inabidi ukaze moyo Maria
usije niache pweke Maria

masikini si kilema
matatizo ya dunia
yapasa kuvumilia

ndio mambo ya dunia
iko siku atatulia
mpenzi wangu vumilia

masikini si kilema
matatizo ya dunia
yapasa kuvumilia

ndio mambo ya dunia
iko siku atatulia
mpenzi wangu vumilia

Chorus
Maria...
Maria vumilia
Maria...
Maria sikia

Verse 3
kwa sababu ya umaskini wetu Maria
kwa watu mpenzi hatuna thamani
kwa sababu ya umaskini wetu Maria
kwa watu mpenzi hatuna thamani

tunaonekana sisi ni kama ma-cartooni
ndio maana hatuwalipi hata harusini
sababu kubwa Maria umaskini
nashindwa Maria kukupeleka kwa salooni
si kosa langu, ajuaye ni manali
Maria wewe wewe, usinikimbia
Maria wowo wowo, usiniwache

masikini si kilema
matatizo ya dunia
yapasa kuvumilia

ndio mambo ya dunia
iko siku atatulia
mpenzi wangu vumilia

masikini si kilema
matatizo ya dunia
yapasa kuvumilia

ndio mambo ya dunia
iko siku atatulia
mpenzi wangu vumilia

subira, yavuta heri
leo mambo ni, shwari
mpenzi, tusiyajali
yale yote wasema
tushikane mpenzi wangu
  mimi na wee...


Share on Google Plus

About Anonymous

He is the CEO of Cityville Mombasa. Reach him on 0728622801 or gangsta6g@gmail.com